Klabu ya Fc Barcelona imeshindwa kupata alama tatu muhimu kwenye mchezo wa Derby ya jiji hilo dhidi ya klabu ya Espanyol baada ya kulazimishwa sare ya goli moja kwa moja.
Wababe hao wa Catalans walifanikiwa kupata bao mapema kabisa kwenye kipindi cha kwanza kupitia kwa beki wa kushoto Marcos Alonso, Na kufanikiwa kuwapa Barca uongozi mpaka mchezo unaenda mapumziko klabu hiyo ilikua mbele kwa bao moja.
Kipindi cha pili kiliendelea huku klabu ya Barcelona ikionekana kuhitaji bao la pili kutokana na kulisakama lango la Espanyol ka kiwango kikubwa, Lakini klabu ya Espanyol walionekana kua watulivu na kuzuia kwa nidhamu ya hali ya juu.
Klabu ya Espanyol walifanikiwa kufanya shambulizi la hatari kwenye lango la Barca mpaka kupelekea kupata mkwaju wa penati na kuwekwa kimiani na Joselu dakika ya 73 ya mchezo, Na kuufanya mchezo kua sare mpaka dakika ya tisini ya mchezo.
Klabu ya Barcelona imeendelea kusalia kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya La liga kwa tofauti ya magoli, Kwani wanalingana alama na klabu ya Real Madrid wakiwa na alama 38 kila mmoja baada ya Real Madrid kudhinda mchezo wa jana.

