Mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid na mshindi wa Ballon Dor mwaka 2022 Karim Benzema anakaribia kuongeza mkataba na klabu hiyo ili aendelee kusalia klabuni hapo.
Mshambuliaji Karim Benzema mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu huu yaani mwezi wa sita mwaka 2023. Hivo klabu ya Real Madrid inahitaji kumuongezea mkataba mchezaji huyo kutokana na ubora ambao amekua anauonesha ndani ya klabu hiyo.
Mshambuliaji huyo ambaye anaelezwa kua kipenzi cha rais wa klabu ya Real Madrid Florentino Perez, Lakini pia klabu ya Real Madrid bado inaona ubora wa mchezaji huyo kuendelea kusalia ndani ya klabu hiyo kwasababu bado wanaona umuhimu wake ndani ya timu hiyo.
Kocha wa klabu ya Real Madrid Carlo Ancelotti amesema kua anatarajia kuona nyota Karim Benzema akisalia ndani ya klabu hiyo kwasababu ni gwiji ndani ya timu hiyo, Pia Ancelotti ameeleza kua mchezaji huyo anapaswa kustaafia klabuni hapo na sio Saudia Arabia.
Klabu ya Real Madrid ipo kwenye hatua za mwisho za kumuongezea mkataba Karim Benzema aendelee kusalia klabuni hapo, Lakini klabu hiyo inapanga kumuongezea mkataba pia gwiji mwingine ndani ya timu Luca Modric kwani ndio mpango wa klabu hiyo kuwaongezea mkataba wachezaji hao.

