Brahim Diaz Kukaa Nje Miezi Miwili

Kiungo wa klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Morocco Brahim Diaz inaelezwa anaweza kukaa nje ya uwanja kwa takribani miezi miwili baada ya kupata majeraha ya misuli katika mchezo dhidi ya Real Sociedad.

Brahim Diaz alifanikiwa kuanza alifanikiwa kuanza katika mchezo dhidi ya Real Sociedad wakiwa ugenini lakini hakufanikiwa kumaliza hata kipindi cha kwanza, Kwani alipata majeraha ambayo yalipeleka kutolewa kutokana na majeraha hayo na nafasi yake kuchukuliwa na Rodrygo.brahim DiazKiungo huyo wa zamani wa Ac Milan amekua na kiwango kizuri tangu ajiunge na Real Madrid akitokea Ac Milan jambo ambalo limefanya kua moja ya wachezaji muhimu ndani ya kikosi cha Carlo Ancelotti, Lakini kwa bahati mbaya majeraha yanaweza kuathiri ubora wake ambao amekua nao.

Kiungo Brahim Diaz anatarajiwa kurudi uwanjani mwezi Novemba kwani jeraha linamuweka nje ya uwanja kwa muda wa wiki nane, Mchezaji huyo anaongeza idadi ya wachezaji wenye majeraha ndani ya timu kwani Real Madrid mpaka sasa ina wachezaji wengi muhimu walio na majeraha kama Alaba, Tchouameni, Camavinga, na Jude Bellingham.

 

Acha ujumbe