Kiungo wa klabu ya Barcelona Sergio Busquets anatarajiwa kubaki ndani ya klabu hiyo kutokana na mazungumzo ambayo yanaendelea baina ya kiungo huyo na klabu yake ya Barcelona.

Taarifa zinaeleza kua Busquets anatarajiwa kukubali kupunguza mshahara wake ndani ya klabu hiyo ili aweze kuongozewa mkataba wa kusalia ndani ya Barcelona, Kiungo huyo amekua kwenye ubora mkubwa ndani ya timu hiyo kwa takibani miaka 15 sasa.busquetsKiungo Busquets alikua akihusishwa kujiunga na ligi kuu ya Marekani mwishoni mwa msimu huu lakini kutokana na mazungumzo ambayo yanaendelea mpaka sasa baina ya klabu na kiungo huyo ni wazi mpango wa kuelekea Marekani unawezekana umekufa.

Klabu ya Barcelona ipo kwenye wakati mgumu kwenye masuala ya fedha kwani mpaka sasa wamefungiwa kusajili dirisha kubwa mpaka wafikishe mapato ya Euro milioni 178, Hivo watahitaji kuhakikisha wanawabakiza wachezaji wake kwa kuwapunguzia mishahara ili waweze kubaki.busquetsSergio Busquets ndio mchezaji mkongwe zaidi ambaye amebakia ndani ya timu hiyo kutoka Barcelona bora kabisa ambayo kocha wasasa wa klabu hiyo Xavi Hernandez alikua mchezaji hivo klabu hiyo inataka kumbakiza klabuni hapo na kumheshimisha kwa kumpa mkataba wa mwaka mmoja au miwili kama taarifa zinavyoeleza.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa