Frenkie de Jong: Barcelona ni Klabu ya Maisha Yangu

Hii inaweza kua taarifa mbaya sana kwa mashabiki wa Manchester United baada ya kiungo wa klabu ya Barcelona Frenkie de Jong kusema hatarajii kuondoka ndani ya klabu hiyo.

Kiungo Frenkie de Jong amesema hatarajii kuondoka ndani ya klabu ya Barcelona na mipango yake ni kuitumikia klabu hiyo kwa muda mrefu zaidi, Huku klabu ya Man United ilikua ikimfuatilia kwa karibu toka msimu uliomalizika.frenkie de jongKiungo raia wa kimataifa wa Uholanzi amebainisha kua anataka kuitumikia Barcelona maisha yake yote ya soka na vilevile hakutaka kuondoka klabuni hapo msimu uliomalizika licha ya matatizo ya kiuchumi yaliyokua yanaikabili klabu hiyo.

Kiungo huyo fundi amesema amekua mshabiki wa klabu ya Barcelona tangu akiwa kijana mdogo, Hivo Barca ni sehemu ya maisha yake na hawezi kufikiria kutimka ndani ya klabu hiyo mabingwa wa soka nchini Hispania.frenkie de jongFundi Frenkie de Jong alikua na msimu bora sana katika msimu uliomalizika baada ya kuanza kwa kutokupata nafasi timu ya kwanza, Lakini alipopata nafasi alionesha ubora mkubwa.

Acha ujumbe