Winga matata wa klabu ya Napoli Khvicha Kvaratskhelia inaelezwa anaweza kua mbadala wa kiungo Jude Bellingham kama akikosekana kwenye dirisha kubwa la usajili ndani ya klabu ya Real Madrid.
Klabu ya Real Madrid imekua ikimuwinda kwa karibu kiungo Jude Bellingham anayekipiga ndani ya klabu ya Borussia Dortmund inaelezwa kua klabu ya Real Madrid inapanga kama ikimkosa kiungo huyo basi watahamia kwa mchezaji Kvaratskhelia anayekipiga ndani ya klabu ya Napoli.Mchezaj Kvaratskhelia amekua kwenye kiango bora sana ndani ya klabu ya Napoli tangu ajiunge klabuni hapo mwaka 2022 akitokea Dinamo Batumi ya nchini Georgia, Mchezaji huyo pia amekua akiwindwa kwa karibu na vilabu mbalimbali barani ulaya kutoka na ubora wake.
Klabu ya Real Madrid imekua ikisajili kikosi cha wachezaji wenye umri mdogo kwasasa kwajili ya kujiandaa na kuondoka kwa magwiji ambao wamekua wakifanya vizuri ndani ya klabu hiyo na ndio sababu wanapambana kutafuta wachezaji wenye umri mdogo ambao wana ubora mkubwa kama Bellingham, pamoja Winga huyo mahiri wa Napoli.Kvaratskhelia ameonesha uwezo mkubwa chini ya Napoli chini ya kocha Luciano Spalletti na kua miongoni mwa wachezaji waliohusika kwenye mabao mengi ndani ya timu hiyo sambasamba na Victor Osimhen, Hiyo ndio sababu kubwa ya klabu ya Real Madrid kumuona kama mbadala kama wakimkosa Jude Bellingham.