Golikipa namba moja wa klabu ya Everton na timu ya taifa ya Uingereza Jordan Pickford amekubali kusaini kandarasi mpya kuendelea kusalia ndani ya klabu ya Everton kocha wa klabu hiyo Sean Dyche amethibitisha hilo.

Golikipa Jordan Pickford amekua kwenye kiwango bora ndani ya klabu ya Everton kwa misimu kadhaa sasa na kumfanya kua moja ya magolikipa bora ndani ya ligi hiyo, Hivo kukubali kusaini dili mpya ndani ya klabu hiyo ni faida kubwa kwa kwa Everton.jordan pickfordKocha Sean Dyche ameeleza kua mchezaji huyo anafurahishwa na uongozi mpya ndani ya klabu hiyo na amekubali ofa ambayo wanakwenda kumpatia golikipa huyo, Lakini pia Sean Dyche amemsifu golikipa huyo kua ni golikipa mzuri na itakua faida zaidi kw aklabu hiyo akiendelea kusalia klabuni hapo.

Golikipa Jordan Pickford amekua akiwindwa na vilabu mbalimbali ndani ya ligi kuu ya Uingereza kutokana na umahiri wake ambao amekua akiuonesha klabuni hapo moja ya vilabu ambavyo viliwinda saini ya kipa huyo ni pamoja na klabu ya Manchester United.jordan pickfordGolikipa huyo namba moja wa ligi kuu ya Uingereza Jordan Pickford ataendelea kusalia ndani ya klabu hiyo kama ambavyo kocha Sean Dyche ameweza kueleza, Hivo ni wazi vilabu vyote ambavyo vilikua vinawinda saini ya golikipa huyo wanapaswa kuangalia mkakati mwingine ili kuweza kupata golikipa mwingine.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa