Laporta: Tunahitaji Kumbakiza Dembele

Rais wa klabu ya Fc Barcelona Joan Laporta amesema kua wana mpango wa kumbakiza nyota wa klabu hiyo raia wa kimataifa wa Ufaransa Ousmane Dembele.

Rais Laporta wakati anazungumza na waandishi wa habari amesema wana furaha na mchezaji Ousmane Dembele na wangependa mchezaji huyo aendelee kusalia ndani ya klabu hiyo, Na ndio maana wanafanya mazungumzo ya kumuongezea mkataba mpya.LaportaKlabu ya Barcelona ipo kwenye mazungumzo na mchezaji Ousmane Dembele kwajili ya kumuongezea mkataba mchezaji huyo, Kwani mkataba wa mchezaji huyo unamalizika mwishoni mwa msimu wa 2023/24 hivo mchezaji huyo amebakiza msimu mmoja ndani ya klabu hiyo kwasasa.

Mchezaji Dembele amekua kwenye kiwango bora ndani ya klabu ya Barcelona tangu kuwasili kwa kocha wa sasa wa klabu hiyo Xavi Hernandez katikati ya msimu uliomalizika na kugeuka kua moja ya mchezaji muhimu ndani ya klabu ya Barcelona chini ya kocha huyo.LaportaRais Laporta amesema Dembele anajua kama klabu inampenda na inahitaji kubaki nae vilevile anajua umhimu wake ndani ya klabu, Kutokana na mazungumzo ya Rais huyo inaonesha moja kwa moja Barcelona wana nia ya dhati ya kumbakiza nyota huyo kwenye viunga vya Camp Nou.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.