Militao Nje Miezi Sita Nje

Beki wa klabu ya Real Madrid Eder Militao atakua nje ya uwanja kwa muda wa takribani miezi sita baada ya kupata majeraha katika mchezo wao wa ufunguzi wa ligi dhidi ya Athletic Club jana.

Beki Militao alipata majeraha jana katika mchezo wa La liga dhidi ya Athletic Club na kupelekea kushindwa kuendelea na mchezo taarifa haikutoka, Lakini leo Real Madrid wameweka wazi mchezaji huyo atakua nje ya uwanja kwa miezi sita.militaoKlabu ya Real Madrid imepata mapigo mawili mazito ndani ya wiki moja kwani mapema wiki hii klabu hiyo ilitangaza golikipa wake namba moja Thibaut Coutois atakosekana uwanjani kwa takribani msimu mzima, Huku leo wakipokea taarifa mbaya tena juu ya beki wao.

Beki huyo raia wa kimataifa wa Brazil ndio alikua chaguo la kwanza kwenye eneo la beki wa kati katika kikosi cha Real Madrid akisaidiana na beki David Alaba atakua nje ya uwanja muda mrefu kwakua lazima afanyiwe upasuaji.militaoBeki Eder Militao amekua kwenye ubora mkubwa ndani ya klabu ya Real Madrid kwa misimu kadhaa sasa na akiisaidia timu hiyo kushinda mataji, Kwasasa itakua ni wakati sahihi wa beki Antonio Rudiger kupata nafasi ya kuingia kikosi cha kwanza.

 

 

Acha ujumbe