Neymar Jr Anukia Al-Hilal

Mshambuliaji wa klabu ya PSG na timu ya taifa ya Brazil Neymar Jr yuko mbioni kujiunga na klabu ya Al-Hilal inayoshiriki ligi kuu nchini Saudia Arabia.

Neymar Jr alikaa mezani na klabu yake ya PSG na kuwaeleza dhamira yake ya kutaka kutimka klabuni hapo, Huku akifanya mazungumzo na Al-Hilal na inaelezwa wako katika hatua za mwishoni na klabu hiyo ya nchini Saudia.Neymar jRMshambuliaji huyo wa zamani wa klabu ya Barcelona ambaye amerudi uwanjani siku za hivi karibuni baada ya kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu alikua anahusishwa na kurejea Barca, Lakini Al Hilal ndio wako mbioni kukamilisha dili hili.

Taarifa zilikua zinaeleza kua mchezaji huyo anaweza kurejea katika viunga vya Camp Nou na kukipiga ndani ya Barcelona, Lakini matatizo ya kiuchumi ambayo yanaendelea kuiandama klabu hiyo imezuia mpango huo.Neymar jRMshambuliaji Neymar Jr kama kila kitu kitaenda sawa kama kilivyo kwasasa basi mchezaji huyo ataungana na mastaa mbalimbali waliotimkia katika ligi ya Saudian League Pro nchini Saudia Arabia.

Acha ujumbe