Kiungo wa klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Ufaransa Aurelien Tchouameni taarifa zinaeleza amezikataa klabu za Liverpool na Bayern Munich ambazo zilikua zinamuhitaji mchezaji huyo.
Vilabu vya Bayern Munich na Liverpool vinatajwa kua vilihitaji huduma ya kiungo huyo na walituma ofa kwa klabu ya Real Madrid, Lakini kiungo Tchouameni amezigomea ofa hizo na lengo lake ni kusalia ndani ya klabu ya Real Madrid.
Kiungo huyo wa kimataifa wa Ufaransa alipoteza nafasi yake ndani ya klabu ya Real Madrid na hiyo ilitokana na kiungo huyo kupata majeraha baada ya michuano ya kombe la dunia mwaka jana mwishoni.
Tchouameni amekua akifukuziwa na vilabu hivo wakitumia faida ya mchezaji huyo kutopata nafasi ndani ya klabu ya Real Madrid, Lakini wamegonga mwamba kwani anaamini anaweza kupambania namba ndani ya timu hiyo.
Klabu ya Real Madrid kwa upande wao pia wameweka wazi kua moja ya wachezaji ambao hawagusiki ndani ya klabu hiyo kiungo Tchouameni ni mmoja wao hivo ni wazi kiungo huyo wa zamani wa Monaco bado yupo sana ndani ya klabu hiyo.

