Vinicius Jr Nje Miezi Miwili na Nusu

Winga wa klabu ya Real Madrid Vinicius Jr anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa muda wa miezi miwili na nusu baada ya kupata majeraha akiitumikia timu yake ya taifa ya Brazil.

Vinicius Jr alipata majeraha katika mchezo uliopigwa juzi Alhamisi wa kufuzu kombe la dunia mwaka 2026 kati ya Colombia dhidi ya Brazil, Mchezaji huyo alielezwa kupata majeraha.vinicius JrWinga huyo tegemezi wa klabu ya Real Madrid alipata majeraha ya misuli ya nyama za paja kama iliyoeleza awali, Ambapo majeraha hayo yatamuweka nje ya uwanja kwa takribani miezi miwili na nusu.

Baada ya kupata majeraha katika mchezo wa juzi mchezaji huyo alisafiri hadi jijini Madrid kufanyiwa vipimo na jopo la madaktari wa klabu hiyo, Baada ya kufanyiwa vipimo klabu hiyo imetoa taarifa juu ya mchezaji huyo kupata majeraha ya nyama za paja zitakazomuweka nje kwa muda mrefu.vinicius JrWinga Vinicius Jr alipata majeraha mwanzoni mwa msimu huu ambayo yalimuweka nje ya uwanja kwa kipindi kifupi, Lakini wakati huu mchezaji huyo atakosekana kwa miezi miwili jambo ambalo litaigharimu klabu yake ya Real Madrid kwani amekua mchezaji muhimu sana klabuni hapo.

Acha ujumbe