Mshambuliaji wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya Uingereza Marcus Rashford bado ameendelea kuchechemea katika michezo mbalimbali ambayo amekua akiitumikia klabu yake na timu ya taifa.
Marcus Rashford ambaye alikua na msimu bora sana katika msimu uliomalizika,Lakini msimu huu ameonekana kutokua kwenye ubora wake kabisa baada ya kushindwa kufanya alichokua akikifanya msimu uliomalizika.Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uingereza ameendelea kuonesha kiwango cha chini hadi kwenye timu ya taifa, Kwani jana wakati akiitumikia timu yake ya taifa bado kiwango chake kimekua sio chga kuridhidha.
Msimu uliomalizika mshambuliaji huyo alifanikiwa kufunga mabao 30 katika michuano yote na kufanikiwa kuingia kwenye timu ya msimu katika ligi kuu ya Uingereza, Lakini msimu huu ukiwa unaelekea katikati bado hajafanikiwa kuonesha kurudia alichokifanya mwaka jana.Marcus Rashford mpaka sasa amefanikiwa kufunga bao moja mpaka sasa kwenye ligi kuu ya Uingereza, Jambo ambalo linatia shaka kwa mchezaji huyo kuanzia kwa klabu yake na timu ya taifa kwani anaweza kupoteza nafasi kwenye timu zake haswa kwenye klabu yake.