Klabu ya Manchester United imeendelea kukubwa na majanga na hiyo ni baada ya golikipa wake namba moja Andre Onana kupata majeraha akiitumikia timu yake ya taifa ya Cameroon.

Andre Onana alishindwa kumaliza mchezo jana wakati akiitumikia timu yake ya taifa ya Cameroon, Hivo hii ni dalili mbaya tena kwa klabu ya Manchester United ambayo inaandamwa na majeraha sana kwasasa.manchester unitedMan United msimu huu wamekua wakiandamwa na majeraha haswa kwa wachezaji wa kikosi cha kwanza, Hivo kuonekana kwa Onana kutoka katika mchezo wa jana akiwa anachechemea ni dalilia mbaya kwa klabu hiyo kuelekea kurejea kwa ligi.

Wiki moja iliyopita imetaarifiwa kua wachezaji wawili wa klabu hiyo Christian Ericksen na Rasmus Hojlund wamepata majeraha ambayo yatawaweka nje ya uwanja kwa siku kadhaa jambo ambalo linaendelea kuitingisha klabu hiyo.manchester unitedKama itathibitika Andre Onana atakaa nje ya uwanja kwa muda itakua ni pigo kwa klabu hiyo tena, Lakini mpaka sasa taarifa rasmi za kua mchezaji huyo atakaa nje kwa muda gani bado hazijatoka huku ikielezwa itakua ni muda wa golikipa wa kimataifa wa Uturuki Altay Bayindir kuweza kupata nafasi ndani ya Manchester United.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa