Manchester United Inaendelea Kufanya Usafi

Klabu ya Manchester United inaendelea kufanya usafi ndicho unachoweka kusema kwasasa baada ya taarifa kutoka kua mkurugenzi wa michezo klabuni hapo John Murtough anajiandaa kuondoka.

Jana taarifa kutoka klabu ya Manchester United zilieleza kua mkurugenzi mkuu wa klabu hiyo Richard Arnold aliachia ngazi klabuni hapo baada ya kukaa klabuni hapo kwa miaka 14.manchester unitedMnunuaji mpya wa hisa klabuni hapo bosi Sir Jim Ratcliffe ambaye anatarajiwa kukamilisha ununuaji wa hisa asilimia 25% inaelezwa ndio yuko nyuma ya mabadiliko yote ambayo yanatokea mpaka sasa klabuni hapo.

Bosi huyo ana mpango wa kuvunja mfumo wote wa uongozi klabuni hapo na kujenga mfumo mwingine kabisa ambao utawaajiri watu wenye uwezo mkubwa wa kuongoza mpira, Kwani lawama nyingi zilikua zikitupwa kwa viongozi klabuni hapo wakionekana kushindwa kutimiza majukumu yao.manchester unitedJean Claude Blanc raia wa kimataifa wa Ufaransa ndio anatarajiwa kua mkurugenzi mkuu mpya wa Manchester United, Huku Paul Mitchell akitarajiwa kua mkurugenzi wa michezo akichukua nafasi ya John Murtough na hao wawili wote ni watu ambao wameshafanya makubwa kwenye vilabu walivyopita.

Acha ujumbe