Son Awatoa Hofu Mashabiki Spurs

Winga wa klabu ya Tottenham Hotspurs Heung Ming Son amewatoa hofu mashabiki wa Tottenham Hotspurs baada ya kuonekana ameumia alipokua anaitumikia timu yake ya taifa.

Son alionekana ameumia katika mchezo kati ya timu ya taifa yake ya taifa ya Korea kusini dhidi ya Singapore, Lakini baada ya mchezo huo amewatoa hofu mashabiki baada ya kusema hakuumia na yupo sawa.sonHofu ilianza kutanda kwa mashabiki wa klabu ya Tottenham baada ya kuona mchezaji huyo ni kama ameumia kwenye mchezo huo, Jambo ambalo limefanya mchezaji huyo kuwatoa hofu mashabiki.

Klabu ya Tottenham kwasasa inaaandamwa na majeraha ya wachezaji wake muhimu, Hivo kama angeongezeka na nahodha wao huyo ingekua taarifa mbaya zaidi kwa klabu hiyo chini ya kocha Ange Postecoglou.sonWinga Heung Ming Son aliiongoza timu yake ya taifa ya Korea leo kupata ushindi wa mabao matano kwa bila mbele ya Singapore, Huku yeye pia akifunga goli moja kati ya mabao hayo matano.

Acha ujumbe