Klabu ya Villarreal imepata pigo kubwa baada ya winga wake raia wa kimataifa wa Hisapnia Yeremy Pino kupata majeraha makubwa yatakayomuweka nje ya uwanja kwa msimu mzima.
Yeremy Pino atakua nje ya uwanja kwa kipindi chote cha msimu kilichobakia kutokana na kupata majeraha ya enka ambayo yatamfanya kukaa nje ya uwanja kwa kipindi chote hicho.Klabu ya Villarreal imethibitisha habari hiyo ya kua winga huyo raia wa kimataifa wa Hispania hatakua sehemu ya timu msimu huu tena mpaka msimu ujao kutokana na majeraha ambayo ameyapata.
Yeremy Pino ni moja ya wachezaji muhimu kwenye kikosi cha Villarreal kwa takribani misimu mitatu sasa, Hivo ni wazi kukosekana kwake kwa msimu uliobakia ni pengo kubwa kwa Nyambizi hao wa njano kutoka nchini Hispania.