Mmiliki wa Klabu ya TP Mazembe, Moise Katumbi amesema tumeingia makubaliano na Klabu ya Simba ili kushirikiana katika mambo mbalimbali yanayohusu mpira.

Katumbi amesema makubaliano ambayo wanayo na Simba ni katika utawala, uchumi na kuuziana wachezaji.

Ikumbukwe kuwa msimu uliopita Simba waliofanya biashara na TP Mazembe ya kuuziana mchezaji Jean Baleke ambaye ameleta chachu kubwa katika mpira wetu kutokana na uwezo wake wa kufumania nyavu

Moise ameishukuru Simba kwa mapokezi yao toka wamefika hapa nchini Tanzania ambapo walikuwa na michezo ya AFL dhidi ya Es Tunis ya Tunisia



JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa