MSEMAJI wa Simba Ahmed Ally amejibu habari zinazosambaa mtandaoni kuwa wanajipanga kwenda kushtaki kwa nembo yao kutumika bila makubaliano yao.
Ahmed Ally alisema, kuna kamati ya sharia itachunguza jambo hilo na kama itaona kuna tija ya kufanya hivyo basi watafanya na kama wakiona hakuna ishu yoyote ya msingi wataachana nayo, huku akisema yota yanayotokea yamesababishwa na wachezaji wao na wanapaswa kujifunza.“Tumeyaona Mabango ya Yanga SC, ila kiukweli haya yote tumeyataka wenyewe sisi Simba SC na haya yote yamesababishwa na wachezaji wetu na wao wanapaswa kuyaona haya mabango.
“Na wakiona Bango limewekwa sehemu kila mchezaji wa Simba SC ajue yeye ndio kasababisha, na ili haya yote yaishe ni mpaka pale tutakapomfunga sisi wenyewe.“Kuhusu kushtaki ipo kamati ya sharia Ambayo itaangalia kama kuna kosa itachukua hatua alisema Ahmed Ally.