SIMBA HAWATASIMAMISHA MCHEZAJI YEYOTE

TAARIFA kutoka ndani ya Simba SC, zinasema hawana mpango wa kuwasimamisha wachezaji wake licha kuwa vyombo vya habari mbalimbali hapa nchini kuripoti kuwa Simba SC ipo kwenye mpango wa kusimamisha baadhi ya vyota wao kwa ajili ya uchanguzi.

Inaelezwa Uongozi wa Simba SC, haina mpango huo huku ikielezwa wanazichukulia taarifa hizo kama sehemu ya propaganda kwa lengo la kukodhoofisha kikosi Chao ambacho kwasasa kina michezo migumu ya CAFCL.SIMBAMmoja wa viongozi wa Simba wamesema: “Hii ni propaganda ambayo kama Simba SC tungeingia basi kikosi chetu kingedhoofika maana Leo hii tuwaondoe wachezaji sita hadi saba wa kikosi cha kwanza unazani tutakuwa na hali gani na kwanini.

“Tuwaondoe sasa wakati ligi inaendelea?, tunachokifanya kwasasa ni kuhakikisha tunatejesha morali yetu ya upambanaji kwenye kikosi chetu, lakini pia huu tumeujua ulikuwa ni mtego na tungefanya hivyo basi kikosi chetu kingedhoofika.

“Lakini pia tumeona kwa wenzetu Yanga SC, wachezaji wao walikuwa na tuhuma kama zinazosemwa kwa wachezaji wetu ila wao walitumia njia gani? waliwafukuza? Hapana Bali walisubiri wakati wa dirisha la usajili na wakafanya usajili kwa maana ya mibadala yao.SIMBA“Na sisi Simba SC kama tutaona Kuna viashiria hivyo japo ni ngumu kumtuhumu mchezaji kufanya jambo kama hilo moja kwa moja maana utatakiwa uwe na ushahidi jambo ambalo litakuwa gumu, ila sisi tutakachokifanya ni kusajili m,badala wa wachezaji hao na sio kuwasimamisha kwasasa.”

Acha ujumbe