Beki wa kulia wa klabu ya Arsenal na timu ya taifa ya Uingereza Ben White amekaribia kusaini kandarasi mpya ya kuendelea kuitumikia klabu hiyo kw amuda mrefu zaidi.

Ben White amekua akifanya mazungumzo na uongozi wa klabu ya Arsenal kwa muda mrefu sasa juu ya yeye kuongeza mkataba wa kuendelea kusalia kwenye viunga vya Emirates.ben whiteKlabu ya Arsenal imekua na utaratibu wa kuwaongezea mikataba wachezaji wake ambao wana mipango nao ya muda mrefu, Kwani mpaka sasa wameshaongeza mikataba kwa wachezaji kama Gabriel Martinelli, Bukayo Saka, Gabriel Malgahes, na William Saliba.

Wiki kadhaa zilizopita ilielezwa kua beki huyo wa kimataifa wa Uingereza ameshafikia makubaliano ya kusaini mkataba mpya na klabu ya Arsenal, Huku kuna baadhi ya mambo madogo yalikua yamebakia kukamilisha dili hili.ben whiteUpande wa beki Ben White na upande wa klabu ya Arsenal mpaka sasa unaamini dili hilo litakamilika, Kwani vitu vya muhimu vyote vimemalizika na yamebakia mambo madogo na ni wazi muda wowote beki huyo atamwaga wino wa kuendelea kuitumikia Arsenal.

 JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa