Tanzania Yaipasua Niger

Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars imefanikiwa kupata matokeo ya ushindi katika mchezo wa kufuzu kombe la dunia ambao wamecheza dhidi ya timu ya taifa a Niger.

Mchezo huo uliopigwa nchini Morocco katika jiji la Marrakech ambapo timu ya taifa ya Niger ndio walikua wenyeji wa mchezo huo, Licha ya kua wenyeji haikuwazuia Tanzania kupata matokeo ya ushindi mbele yao.tanzaniaMchezo huo ulikua wa ushindani huku timu zote mbili zikionekana kuhitaji alama tatu muhimu, Lakini ni vijana wa Taifa Stars waliofanikiwa kupata alama tatu muhimu katika mchezo huo.

Kijana Charles M’mombwa ndio aliehakikisha Taifa Stars wanapata alama tatu baada ya kufunga bao dakika ya 57 ya mchezo ambalo limeweza kudumu mpaka dakika ya mwisho ya mchezo na kuwafanya Taifa stars kuibuka kidedea.tanzaniaTimu ya taifa ya Tanzania baada ya kucheza mchezo wao leo dhidi ya Niger nchini Morocco leo, Lakini watatakiwa kusafiri kurudi nchini kuja kumenyana na timu ya taifa ya Morocco mchezo wa kufuzu kombe la dunia utakaopigwa jijini Dar-es-salam wiki ijayo.

Acha ujumbe