Mwenyekiti wa Tottenham, Daniel Levy atamruhusu straika wa Uingereza Harry Kane 26 kwenye Manchester United kwa dau la £200m ili kupata haueni kiuchumi.
Manchester City wapo tayari kuipiku Chelsea, Real Madrid na Barcelona kumnasa straika wa Argentine, Lautaro Martinez kwa ada ya £97.5m.

Newcastle wanavutiwa kumsaini kiuno wa Ureno Rafa Silva, 26 kutoka Benfica, lakini mazungumzo yamesimama kutokana na mlipuko wa Corona.
Manchester City wanahitaji kumsajili beki Boubacar Kamara, 20 na Marseille wapo tayari kumuachia mfaransa huyo kwa £28m.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Ulaya, Uefa linaamini linaweza kumaliza msimu wa Ligi ya Mabingwa na Ligi ya Europa kwa wiki tatu mwezi Agosti.
Sky Sports wamekiri kuwa hawahitaji Ligi Kuu ya Uingereza iwalipe £371m kama msimu utafutwa kutokana na janga la Corona.
Wakala wa James Rodriguez amezungumza na Manchester United na Juventus okama wanaweza kumsajili kipindi cha majira ya kiangazi kutoka Real Madrid.
Vilabu vya Uingereza vinamuwinda beki wa RB Leipzig Dayot Upamecano – ikiwemo Arsenal, Tottenham na Manchester City.


Fatina mfingi
Asanteh kwa taarif merdiana bet