Wakati ufunguzi rasmi wa dirisha la usajili ukikaribia mwishoni mwa wiki hii, dau la Darwin Nunez linatajwa kuzigonganisha Liverpool na Manchester United.

Nani mwenye nguvu ya pesa na ushawishi sokoni? Matakwa ya wachezaji ni yapi? Ni usajili wa muhimu au ni kutishana sokoni? Songombingo za usajili ni nyingi sana sokoni, nani ni nani ndani ya miezi 2 ya usajili?

Baada ya Newcastle United kushindwa kumsajili Darwin Nunez mwezi Januari, dau la mchezaji huyo limepanda maradufu majira haya ya kiangazi. Benfica wamemuwekea thamani ya €100M kwa timu yeyote inayotaka kumsajili kwenye dirisha hili.

Inaaminika Nunez mwenyewe ameweka akili na mawazo yake yote kwenye soka la Uingereza msimu ujao. Swali ni kwamba, kunatimu itafikia dau la Benfica.


Jurgen Klopp (kushoto) akipongezana na Erik Ten Hag (kulia)

Japokuwa Manchester United wanajulikana kwa kumwaga pesa kwenye soko la usajili, mpaka sasa hawajulikani ni kitu gani wanakitaka licha ya kuwa na msimu mbovu zaidi kwenye historia ya klabu hiyo.

Ujio we Erik Ten Hag na uongozi mpya chini ya Richard Arnold, unaonekana kama mwanzo mpya kwa United. Kulikua na taarifa kuwa United ilishaanza mazungumzo na Benfica kuhusu Nunez lakini, baadae walisimamisha mazungumzo hayo na kuweka nguvu zaidi kwenye kumsaka kiungo mpya wa klabu hiyo.

Pengine kuzubaa kwa United kunawapa nafasi Liverpool ambao wametajwa kuingia kwenye kinyang’anyiro cha kumsajili Nunez. Jurgen Klopp anavutiwa sana na mchezaji huyu ambaye aliwafunga nje ndani walipokutana kwenye Ligi ya Mabingwa msimu ulioisha. Ni Liverpool au United atakayefanikiwa?


Bila shaka unatamani ushindi mkubwa, vipi kuhusu kujaribu Sloti hii ya Aliya’s Wishes? jaribu ushinde sasa.Kasino ya Mtandaoni

CHEZA SASA


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa