Robert Lewandowski amekuwa sikio la kufa juu ya kubadili mawazo yake ya kutaka kuondoka Bayern Munich msimu huu wa joto. Inaonekana kuwa Barcelona ndiyo sehemu anayopanga kwenda kwa sasa ikiwa ataondoka.

Taarifa zinasema kuwa, licha ya Barcelona kujaribu kufanya kila namna kumpata staa huyu, Barca pia wanaweka mpango wa kando wa kumpata mbadala wake ikiwa watamkosa nyota huyu.

Kwenye mpango huu wa kando Gerard Moreno anatajwa kuwa lengo la Barcelona, ikiwa watakosa mlengwa wao wa awali. Nyota huyu amekuwa na mchango mkubwa Villarreal, akiwasaidia kushinda Europa League na pia kutajwa kwenye orodha ya wachezaji waliowania Ballon d’Or.

Mpango wa Kando wa Barcelona Wakimkosa Robert Lewandowski
Gerard Moreno

Villarreal wanatajwa kuwa wapo tayari kupokea dau la takribani €40m kwa Moreno, ambaye mkataba wake unafika hadi mwaka 2027. Gharama hii inafanana na gharama ambayo Barcelona wanaweza kutumia kwa Robert Lewandowski.


Bila shaka unatamani ushindi mkubwa, vipi kuhusu kujaribu Sloti hii ya Aliya’s Wishes? jaribu ushinde sasa. Kasino ya Mtandaoni

CHEZA SASA

 

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa