Michezo imekuwa sehemu muhimu sana ya historia ya mwanadamu na maendeleo yake. Imetumika zaidi na wazee wa kale kama namna ya kutoa mafunzo kwa vijana wao wakati wa kukua. Je ipi ni mechezo ya kwetu Tanzania na Afrika kwa ujumla iliyokuwepo kabla ya ukoloni?

Kwa sasa, matokeo ya ukuaji wa sayansi na teknolohia pamoja na mchango fulani wa tamaduni za wakoloni, tumekuwa wapenzi wa michezo mingi zaidi ya kisasa. Soka likionekana kuwa na mashabiki wengi zaidi Afrika.

Kabla ya ujio wa wakoloni kuna michezo iliyobamba zaidi Afrika. Hapa tunakuletea baadhi ya michezo ya wakati huo ikiwa ni pamoja na michezo ifuatayo;

Ta Kurt Om El Mahag – Libya

Huu ni mchezo unaofanana na mchezo wa Baseball, ni mchezo maarufu katika makabila la Berber huko Libya. Hadithi zinasema kuwa mchezo huu ulichukuliwa na watu wa Ulaya wakati wa zama za Mawe kisha ukapewa jina la Baseball baadaye.

Mchezo wa Fimbo wa Wangoni, Kusini mwa Afrika

Huu ni mchezo wa kupigana kwa fimbo ambao ulichezwa na jamii za wangoni. Mchezo huu una historia kubwa sana kusini mwa Afrika. Mchezo huu ulikuwa unaweza kuchukua hadi masaa matano, wachezaji wakibadilishana zamu ya kujilinda na kushambulia na walipata pointi za ushindi. Huu ni moja ya michezo hatari zaidi na wachezaji wanaweza kufa. Mchezo huu ulishazuiliwa lakini bado unachezwa sehemu chache kusini mwa Afrika.

Michezo ya Waafrika Kabla ya Ukoloni

Bao – Afrika Mashariki

Bao ni mchezo maarufu sana kwa upande wa pwani ya Afrika mashariki, na hadi sasa mchezo huu umekuwa ukichezwa kwenye ukanda huu. Mchezo huu ulikuwa maarufu miaka mingi iliyopita kwa nchi za Tanzania, Congo, Kenya, Malawi na Burundi. Umaarufu wake ulikuwa mkubwa hasa kwa jamii za waswahili na pwani. Mchezo huu una historia muhimu katika kutafuta uhuru wa Tanzania, wakati viongozi wa wakati huo wakiketi mabarazani na kubadilishana mawazo.

Dambe – Ndondi, Hausa – Nigeria

Huu ni mchezo wa masumbwi, ambao wapiganaji wake walisafiri vijiji tofauti tofauti msimu wa mavuno ikiwa kama moja ya burudani za wakati buo. Mkono mmoja unakuwa umefungwa na kamba kwa wapambanaji, na pambano linawaka moto mpaka mmoja anapoanguka chini.

Mbio za Punda, Lamu – Kenya

Huu ni mchezo maarufu huko Lamu, nchini Kenya. Wakati kukiwa hakuna magari kwenye kisiwa hiki, mbio za kila mwaka ziliandaliwa na utawala. Wapambanaji wanahitaji utaalamu kukimbia na punda ambao wamefunzwa vyema. Mchezo huu umeishi kwa karne nyingi sana.

Donkey Lamu Kenya
Mbio za Punda, Lamu, Kenya 2010, Photo credit: Xiaojun Deng via Flickr

Laamb – Mieleka – Senegal

Huu ni mchezo wa miaka mingi sana, ulikuwa unawahusisha wavuvi na wakulima wa Senegal. Mchezo huu bado una ushawishi mkubwa zaidi na wapambanaji wanalipwa pesa nyingi sana hadi dola laki moja kwa pambano. Ni mchezo unaotoa ushindani kwa Soka kwa kuwa maarufu Senegal.

Hii ni baadhi ya michezo maarufu. Michezo ipo mingi sana kwenye historia.


ALIYA’S WISHES

Bila shaka unatamani ushindi mkubwa, vipi kuhusu kujaribu Sloti hii ya Aliya’s Wishes? jaribu ushinde sasa. Kasino ya Mtandaoni

CHEZA SASA

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa