Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Manchester United Robin van Persie alimwambia Erik ten Hag hawezi kupata klabu bora ya kuifundisha ispokuwa klabu hiyo ya mashateni wekundu kabla ya kukataa kazi ya kuwa msaidizi wake.

Erik ten Hag alihitaji mchezaji huyo wa zamani wa klabu ya Arsenal na Man Utd awe msaidizi wake kwenye viunga vya Carrighton Park lakini Robin van Persie alikataa kurudi Old Trafford. Kabla ya Ten Hag kuwachukua Mitchell van der Gaag na Steve McClaren.

Robin van Persie

Lakini Robin van Persie aliamua kubaki kwenye nafasi yake kama kocha wa timu ya kwanza na vijana kwenye klabu Feyenoord, ambapo mtoto wake wa kiume mwenye miaka 15 anacheza. Japo kulikuwa na nafasi ya kurudi kwenye viunga vya Old Trafford.

“Heshima ya mashabiki ni kubwa mno, Van Persie alisema. “Niliporudi miaka michache iliyopita nikiwa na Fenerbahce, baada ya kushinda ubingwa wa ligi kuu na Man Utd nikiwa chini ya Sir Alex, bado ninakubaliki pakubwa na watu.

Robin van Persie, Robin van Persie Aelezea Sababu ya Kuikacha kazi Man Utd, Meridianbet

“Dick, kocha wetu wa  Fenerbahce, anatambua hilo. Ameshapata uzoefu huo akiwa Rangers ya Scotland. Alliniambia kwa maisha yako yote utakubalika hapa { Man Utd} na alikuwa sahihi kabisa.

“Uingereza ni nchi nzuri kuishi. Watu wake wakarimu na ni marafiki. Ni dakika 40 kutoka Rotterdam kwa ndege , lakini unaishia kwenye dunia nyingine taofauti kabisa, Sehemu nzuri duniani.

“Soka lilinifaa sana.  Bado nadhani ni ligi inayovutia duniani. Viwanja vyake ni kijana kama uwanja wa pool Tables. Viwanja vyake  vyote vikubwa  na vinajaza na hakika uingereza wanapumua kwa sababu ya mpira.

“Watoto wangu na familia yangu ni muhimu kwa sasa, jambo la muhimu wote wamejua nini wanataka kwa sasa, lakini matumai wamepata wanavyovutiwa navyo. Nilipokuwa nacheza Arsenal , nilihama mara tano.

“Pia nimeishi Manchester na Istanbul. Yote kwa yote, Tumekuwa nje ya nchi kwa miaka kumi na nne. lakini sasa tinafikilia nini kizuri kwa watoto wetu ? na tunahisi kidogo hapa kutakuwa pazuri.” Alisema Robin van Persie.


SHINDA SAMSUNG A32 NA AVIATOR

SHINDA Samsung A32 ukiwa na mchezo wa Aviator kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet! Kwea pipa ukusanye zawadi zako pamoja na ushindi mnono wa mkwanja!

kasa wa njano, Kasa wa Njano Awapa Ubingwa wa CL Liverpool., Meridianbet

SOMA ZAIDI HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa