Uchambuzi Mechi Kati Ya Athletic Bilbao vs Real Madrid.

Real Madrid wataendelea kuzitafuta alama tatu kuendelea kuongoza katika  msimamo wa La liga pale watakapo safiri siku ya Jumapili mpaka Athletic Bilbao walio katika kiwango kizuri.

Los Blancos wanaongoza ligi ya LaLiga kwa tofauti ya alama nne juu ya Barcelona walio katika nafasi ya pili, wakati Athletic Bilbao wapo katika nafasi ya nane, alama nne wamezidiwa na Getafe waliyo katika nafasi ya sita  katika mbio za kushiriki kucheza Europa League msimu ujao.

Athletic wamekuwa katika fomu tangu kurejea kwa michezo baada ya kusimama kwa muda, wameshinda michezo mitatu wametoa sare mbili na kupoteza mchezo mmoja katika michezo sita iliyochezwa.

Upande wa Gaizka Garitano kwa sasa wapo katika nafasi ya nane, alama nne nyuma ya Getafe ambao wapo katika nafasi ya sita  ambao pia wana michezo na Villarreal, Sevilla, na Atletico Madrid.

Athletic wamekuwa wakipata matokeo katika uwanja  nyumbani kwa msimu huu, kwani wameshinda michezo tisa kati ya kumi na sita wakichuana vikalina wababe wa Spain kama Real Madrid, Atletico Madrid na Barcelona.

Athletic hawajawafunga Los Blancos tangu mwaka 2015 igawa kwenye michezo minne iliyopita walikwenda sare.

Wakati huo huo Real Madrid mameshinda michezo yote sita, Zinedine Zidane amezifunga timu kama Eibar,Valencia,Real Sociedad, Mallorca, Espanyol na Getafe waliowafunga katika dakika ya 79 kwa penati siku ya Alhamisi.

Real Madrid watajihakikishia nafasi ya kuchukua taji la La Liga kama watafanikiwa kuwafunga Athletic Bilbao huku dua likiwa Barca wapoteze mchezo wao dhidi ya Villarreal.

Ni vigumu kuona Los Blancos wakishindwa kupata pointi kwa michezo yao minne iliyo salia, michezo hiyo watakabiliana na Alaves, Granada, Villarreal na  Leganes.

Kwenye mchezo wa leo Athletic Bilbao watamkosa nyota wao Benat, kutokana na tatizo la paja kwa upande wa Madrid wanaweza kumkosa Raphael Varane kwa kuwa na jeraha kichwani lililopelekea kutoka nje kwenye mchezo dhidi ya Getafe siku ya Alhamisi.

Nacho anaonekana kama hatocheza kutokana na majeraha yanayo mkabili, lakini Eden Hazard anaweza kucheza ingawa mchezo uliopita alipumzika.

Athletic Bilbao Kikosi kinachoweza kuanza:                                                           Simon,Capa, Yeray, Martinez, Yuri; Lopez, D Garcia; Muniain, R Garcia, Cordoba; Williams

Real Madrid kikosi kinachoweza kuanza:                                                              Courtois; Carvajal, Varane, Ramos, Mendy; Kroos, Casemiro, Valverde; Hazard, Benzema, Isco

 

 

47 Komentara

    Safii Sana makara nzuri

    Jibu

    Madrid bado ananafasi kubwa ya kushinda kwenye hii mechi

    Jibu

    Bonge la game hii ni draw ya magoli

    Jibu

    Hii game cwez kukosa

    Jibu

    Duuh hapo tuombe sijui nani atakua mshindi

    Jibu

    Litakuwa bonge la mechi ili real wanatakiwa washinde ili wajikite kileleni

    Jibu

    GG3+ iyo game ..

    Jibu

    Ni mechi nzuri sana mpambano utakuwa sio wa kawaida kwa wachambuzi wachambue kwa makini sana sio masiala

    Jibu

    Bonge la Darb dk 90 ndizo zitakazo amua.

    Jibu

    Sio ya kukosa

    Jibu

    Dakika 90 mshindi atapatikana tu ila ubashiri wangu nampa real Madrid

    Jibu

    Bonge la mechi ila real Madrid wakishinda watazidi kuwa katika nafasi nzuri

    Jibu

    Madrid hamna kitakachowafanya wasikombe point 3 leo wazidi kuukaribia ubingwa wa la liga

    Jibu

    Seriously game ngumu sana hii

    Jibu

    Real Madrid inacheza kufa na kupona mechi za lala salama.Real inahitaji ubingwa kuliko timu yoyote sasa hivi #meridianbettz

    Jibu

    Hii mechi itakua ngumu kidogo kwa Madrid lakin zidane atafanya jambo

    Jibu

    Don’t miss. MADrid gar limewaka

    Jibu

    Hii mechi tusubili matokeoa tu.

    Jibu

    Mechi itakua ngum ila Madrid Kwa sasa awana chakupotez

    Jibu

    Tusubiri matokeotu kwani hii mechi ningumu

    Jibu

    Good new

    Jibu

    Maoni:Daah mechi itakua ngumu sana hiyo

    Jibu

    madridi ana nafasi nzur ya kushinda na atashinda

    Jibu

    Mechii kubwaa hii

    Jibu

    Itakua big match

    Jibu

    Real Madrid inatafuta ubingwa kwa nguvu zote Nina Imani mechi hii anashinda

    Jibu

    Makala inaeleweka mno

    Jibu

    Ahsanten meridian makala iko poa kinoma , lkn mwamuz ni dk 90 uwanjan Nani kuwa kidedea?

    Jibu

    Uchambuzi ulikuwa mzuri Sana maana ulikuwa unalenga kabisa uhakisia wa mechi husika

    Jibu

    game tough

    Jibu

    Yaani Mie Kila Siku ni Kuwaombea Madrid Ushindi#Meridianbettz

    Jibu

    Maoni:hiyo ndio soka kabambe

    Jibu

    Hii si ya kukosa kabisa sijui nani atatoka mshindi wote wakali

    Jibu

    Madrid wako vizuri sana msimu huu

    Jibu

    Athletic bilbao kwa leal Madrid cha mtoto tu wasubir kuhesabu magoli asilimia mia

    Jibu

    sisi mashabiki wa atletico tunacomment wapi

    Jibu

    Hii gemu siwezi kuikosa

    Jibu

    Mambo ni moto

    Jibu

    Madrid wanashinda#meridianbett

    Jibu

    Axante kwa taarifa

    Jibu

    Madrid bado ananafasi kubwa kushinda mechi hii

    Jibu

    Madrid babalao ajawahi kukosea

    Jibu

    Ni vigumu kuona Los Blancos wakishindwa kupata pointi kwa michezo yao minne iliyo salia, michezo hiyo watakabiliana na Alaves, Granada, Villarreal na Leganes.

    Jibu

    Mechi hii nasubiri kwa hamu sana

    Jibu

    Uko poa sana 👍

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.