Mshambuliaji wa klabu ya Manchester United na raia wa Ufaransa Anthony Martial huenda akachukua nafasi ya Christopher Nkunku baada ya kupata majeraha kwa mchezaji huyo katika kambi ya timu ya aifa ya Ufaransa.

Mapema jana ilitoka taarifa rasmi kutoka kambi ya timu ya taifa ya Ufaransa juu ya kuumia kwa mchezaji Nkunku na anatarajia kuikosa michuano hiyo inayotarajiwa kuanza Novemba 20 nchini Qatar.martialMchezaji Nkunku amepata majeraha akiwa kwenye mazoezi ya timu ya taifa ya Ufaransa wakati akiwa anagombea mpira na Eduardo Camavinga na kumsababishia majeraha ya goti mchezaji huyo na kukosa nafasi ya kushiriki michuano hiyo.

Baada ya Nkunku kukosa michuano hiyo anahitajika mshambuliaji wa kuziba pengo la Nkunku na Martial anazungumzwa kama mrithi wa mchezaji huyo kwenye kikosi cha kocha Deschamps.martialMshambuliaji Martial licha ya kuandamwa na majeraha muda mrefu ndani ya msimu huu lakini kila ambapo amekua akipewa nafasi ya anaonesha ubora mkubwa katika timu ya mwalimu Eric Ten Haag na ndio anapewa nafasi ya kuziba nafasi ya Christopher Nkunku.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa