Mchezaji wa timu ya Taifa ya Marekani Yunus Musah anaamini kuwa ulimwengu mzima utauona ubora wa Marekani baada ya kuwabana Uingereza kwa sare tasa katika mechi ya pili kwenye Uwanja wa Al Bayt hapo jana.

Uingereza inachukuliwa kuwa miongoni mwa timu yeynye wachezaji wanaopendekezwa kutwaa taji la Kombe la Dunia, lakini walikuwa kwenye wakati mgumu hapo jana baada ya kupata mpinzani mgumu na kushindwa kupata ushindi.
Marekani ambayo ina wachezaji kama Christian Pulisic ilikuwa ni ngumu kupata matokeo kutokana na ubora ambao waliuonyesha hapo jana na kupeleka mashmbulizi ya hatari langoni kwa Uingereza.
Musah alihisi matokeo ya sare ni ya haki, lakini kijana huyo ambaye alistahili kuchezea Uingereza bado alifurahishwa na uchezaji wa Marekani akisema kuwa ni mchezo ambao walituma ujumbe na kusema kuwa timu yao imecheza vizuri sana na kuonyesha jinsi walivyo.

Musah alisisitiza kwa kusema kuwa wengi wao wanacheza katika timu kubwa kwa kiwango cha juu, na anahisi kama Ulimwengu wote utaona Marekani inaweza kufanya mambo mazuri
Muda utasema hawawezi kuishi kwa mchezo mmoja tu, lazima wafanye hivyo mara kwa mara. Marekani ina vijana ambao ni miongoni mwa wanaopewa nafasi kubwa kushinda mashindano.
Mafanikio ya Marekani ya kupata sare hapo jana na kuwaaibisha Uingereza yalidhihirika kwa jinsi Three Lions walivyozomewa baada ya filimbi ya mwisho, na Pulisic aliongeza: “Nadhani hiyo ni ishara chanya unapoichezea timu nyingine, ulikuwa ni mchezo mzuri sana.”

Pulisic alikazia kwa kusema kuwa mashabiki pinzani hawapendi kuliona hilo hasa wanapokuwa vijana wa chini lakini walienda nao sambamba na kufanya vizuri, huku Marekani wakiwa hawajashinda hata mchezo mmoja na sasa wanaelekezea nguvu zao kwa Iran ambayo imeshinda dhidi ya Wales.
Musah amemalizia kwa kuangazia jinsi Iran walivyowakabili Wales na kusema kuwa wamepigana sana hata uchezaji wao ulikuwa wa kukimbia na kukimbia na kushinda kutokana na juhudi. Wao wanapaswa kuwa tayari na kujiandaa kwani hamna timu ndogo kwenye Kombe la Dunia.

Je wewe hucheza Kasino Mtandaoni na umekuwa ukijiuliza ni mchezo gani rahisi na mzuri kwa ushindi? Basi Usihangaike Aviator ni rahisi zaidi kucheza na kushinda, kingine cha zaidi ni kwamba Aviator Bonanza imerudi tena Cheza zaidi ujiweke kwenye nafasi ya kushinda Samsung A23.
BONYEZA HAPA KUCHEZA


