Kiungo wa Tottenham anahusishwa na kujiunga na klabu ya Juventus baada ya kuwa na fununu kwa kipindi kirefu kwamba Madrid walikuwa wakihitaji kumsajili nyota huyo baada ya ripoti kutoka upande wa pili kuanza kufifia. Eriksen amewindwa na klabu hiyo ya Hispania kwa kutengewa madau tofauti lakini jambo hilo halijaweza kufanikiwa kabisa.
Bayern Munich inaonekana inajishughulisha sana sokoni msimu huu kwa kuanza kuhusishwa na kumuwinda nyota wa Barcelona, Coutinho. Klabu hiyo inaonekana kutaka kuwashawishi matajiri hao kama wanaweza kumtoa nyota wao kwa mkopo ili aweze kujiunga na klabu yao hiyo ili aweze kuwasaidia kwenye mashindano makubwa mbeleni japo Barcelona waliweka wazi kwamba nyota huyo hawezi kuondoka kwa sasa.
Baada ya kuhudumu kwa kipindi kirefu na kupata muda mchache sana wa kupata namba ndani ya kikosi cha kwanza cha Liverpool, Daniel Sturridge anaangalia uwezekano wa kutimka kikosini hapo ili kutafuta eneo ambalo ataweza kupata muda wa kutosha. Ameanza kuhusishwa na kujiunga na Fenerbahce ya Uturuki mbali na klabu nyingine 13 kuonesha nia ya kutaka kufanya naye kazi.
Sakho amegeuka kumshauri mchezaji mwenzake Wilfred Zaha kwa kumuambia aweke kando tofauti zake na matajiri wa klabu hiyo na kugeukia upande wa pili kuonesha kiwango cha kipekee zaidi uwanjani ili asipotee sokoni. Ikumbukwe Zaha alijitahidi kuweka ushawishi mkubwa ili kutimka kikosini hapo jambo ambalo liligonga mwamba na hakufanikiwa kuondoka klabuni hapo katika usajili.
Klabu ya Inter Milan inaonekana kujibiidisha sana kujenga kikosi chao kwa ajili ya ushindani zaidi hapo baadaye. Kwa sasa tayari wameweka malengo yao ya kumshusha Edinson Cavani mara baada ya kandarasi yake kuisha ndani ya PSG. Vigogo hao tayari wamefanya usajili mkubwa hadi sasa ikiwa ni hatua ya pekee kujiimarisha.
Nyota wa Real Madrid na raia wa Wales, Gareth Bale anaonekana kuwa njiapanda kwenye timu hiyo baada ya kurudi kwa zile fununu zilizokuwa zikimhusisha na kutimkia China. Taarifa zinadai kwamba kuna mambo mawili yataamua soka lake Hispania ama yeye kutimkia China baada ya kufunguliwa kwa dirisha au aombee Zidane afutwe kazi ndani ya timu hiyo.
Povel
Habar njema