Kocha mkuu wa Paris Saint German Christophe Galtier amethibiisha kuwa kutukanwa kwa Kihispania ndio ilikuwa sababu kuu ya beki wake Sergio Ramos Kupewa kadi nyekundu hapo jana kwenye mchezo dhidi ya Reims.

Christophe na vijana wake walikuwa ugenini hapo jana na walitoa sare ya bila kufungana, hivyo ikiwa ni sare ya pili mfululizo baada ya kutoa nyingine kwenye mchezo uliopita wa ligi ya Mabingwa dhidi ya Benfica.
Ramos alipata kadi mbili za njano baada ya muda mfupi kabla ya mapumziko na kuwaacha Psg wakiwa kumi uwanjani huku kadi hiyo ikitokana na kugombana vikali na mwamuzi wa mchezo huo.

Ramos ambaye ni Mhispania ametimuliwa nje kwa mara ya 21 katika maisha yake ya soka akiwa Laliga pamoja na Ligue 1. Akizungumza baada ya sare hiyo, ambayo inaifanya Psg iiache Marseille kwa pointi tatu kileleni, kocha huyo alisisitiza kuwa anaamini kuwa beki wake Ramos hakukusudia kumkera Gaillouste.
“Ninamfahamu vyema Sergio Ramos, sina uhakika kuwa tusi lililotoka lilielekezwa kwa mwamuzi,” Galtier alisema.


