Glazers Kumbania Ole Gunnar Bajeti ya Usajili

Wamiliki wa klabu ya Manchester United, Familia ya Glazers wanaripotiwa kuwa hawajajiandaa kumpatia meneja Ole Gunnar pesa kwa ajili ya usajili wa dirisha la mwezi Januari.

Licha ya kutumia pesa kubwa kwa ajili ya usajili wa Cristiano Ronaldo, Jadon Sancho na Raphael Varane, matarajio ya klabu yanaonekana kuendelea kubuma chini ya Ole Gunnar.

Matokeo mabaya yanaendelea kumpa shinikizo Ole Gunnar, ambaye anaonekana kuwa karibu kukalia kuti kavu baada ya wachezaji kadhaa wakubwa kuripotiwa kuwa wanataka meneja huyu aondoke klabuni hapo.

Ole Gunnar

Kusalia kwa Ole mpaka sasa ni kwa sababu ya uhusiano wake mzuri na wakubwa wa Man United, ambao wana matumaini meneja huyu anaweza akapindua meza na kurejea kwenye njia ya ushindi.

Kwa mujibu wa The Mirror, Familia ya Glazer, haina imani kuwa dirisha la Uhamiso la mwezi Januari linaweza kubadilisha changamoto iliyopo klabuni hapo, na hivyo hawatatoa fedha kwa ajili ya usajili.

Ripoti zinaeleza zaidi kuwa Ole Gunnar hajioni hata kidogo akiwa kwenye hatari ya kupoteza kibarua chake kwa sasa.

United wamepoteza gemu nne kati ya gemu sita zilizopita za EPL chini ya Ole na wanajiandaa kuvaana na Watford baada ya likizo ya kimataifa.


NJIA RAHISI YA MKWANJA NA TITAN DICE

Unawezaje kuikosa hii! njia rahisi ya kutengeneza mkwanja katika kasino maridhawa za meridianbet. Muda wa kufurahia na kutengeneza mkwanja ipo mikononi mwako unasubiri nini?

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA SASA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.