Gomes Kutest Mitambo Mingine Mechi 3 Zilizobaki

Baada ya kuchukua ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara msimu huu wa 2020/2021, Kocha wa timu wa msimbazi Didier Gomes ametangaza kupumzisha baadhi ya wachezaji ambao wametumika sana msimu huu na kujaribu wengine.

Akizungumza na waandishi wa habari, Gomes alidai kuwa imefikia kipindi sasa kuanza kutazama uwezo wa wachezaji wengine ambao wamekuwa wakikosa namba kikosi cha kwanza kutokana na ukubwa wa kikosi hicho.

Baada ya kujihakikishia kutetea ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa mara ya nne mfululizo Kocha Mkuu, Didier Gomes amesema atawapumzisha baadhi ya wachezaji waliotumika sana na kuwapa nafasi wengine.

Gomes amewataja nyota hao Miraji Athuman, Said Ndemla, Gadiel Michael na David Kameta kuwa wanafanya vizuri mazoezini na anafurahi kufanya nao kazi lakini kutokana na ukubwa wa kikosi wameshindwa kupata nafasi.

Didier amesema msimu ulikuwa mrefu na wachezaji walipambana na kufanikisha tunatetea ubingwa hivyo kwenye mechi tatu za ligi zilizosalia atawapa nafasi nyota wengine ambao hawajacheza mara nyingi.

“Tunashukuru tumefanikiwa kutetea ubingwa wetu, nadhani tutawapumzisha wachezaji waliocheza mechi nyingi na kuwapa nafasi wengine sababu msimu ulikuwa mrefu.

“Katika mechi tatu za ligi zilizobaki tutawapa nafasi wachezaji ambao hatukuwatumia sana. Simba ni familia ukipanga kikosi bado unakuwa na wachezaji 10 ambao ni bora lakini wanakosa nafasi hivyo ni wakati wao huu,” amesema Gomes.

Baada ya ushindi wa mabao 2-0 tuliopata jana dhidi ya KMC tumejihakikishia kutetea ubingwa kufuatia kufikisha alama 76 ambazo zinaweza kufikiwa na anayefuatia lakini tumemzidi uwiano wa mabao ya kufunga.

Simba imebakisha mechizo mitatu ya kiporo kabla ya ile fainali ya kibingwa ya Kombe la Shirikisho la Azam dhidi ya Yanga. Mechi hizo ni dhidi ya Coastal Unioni tarehe 11, dhidi ya Azam tarehe 14 na dhidi ya Namungo tarehe 18.


KUSANYA PESA HAPA!

IcyGems kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet. Ndio, ukiwa kwenye nyumba ya mabingwa, ndipo utakapoufurahia ubora wa Kasino ya Mtandaoni sambamba na kushinda kwa ushindi mkubwa! Ishi na hii, IcyGems!Meridianbet

INGIA MCHEZONI

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.