Kiungo wa FC Bayern Munich, Leon Goretzka, anaingia kwenye dirisha la usajili akiwa mmoja wa wachezaji wanaowaniwa zaidi barani Ulaya, huku klabu kadhaa zikianza kupigana vikumbo kumpata. Ripoti zinaonyesha kuwa Fenerbahçe wameweka mezani ofa kubwa inayoweza kubadili kila kitu.

Fenerbahçe wanatajwa kuwa tayari kumpa Goretzka mkataba wa miaka mitatu pamoja na ada ya usajili (signing bonus) ya euro milioni 10, jambo linaloonyesha dhamira yao kubwa. Pia wanapanga mazungumzo na kocha Domenico Tedesco kama sehemu ya kumshawishi nyota huyo wa Ujerumani kujiunga nao.
Hata hivyo, ushindani ni mkali. AC Milan nao wameingia vitani wakimpa ofa ya miaka mitatu na mshahara wa takribani euro milioni 5 kwa mwaka pamoja na bonasi. Kocha Massimiliano Allegri anaripotiwa kumtaka sana Goretzka kama chaguo lake kuu la kuimarisha safu ya kiungo.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Kutoka England, Arsenal wanaonekana kuwa mbele kwenye mbio hizi, hasa kutokana na uhakika wa kushiriki Ligi ya Mabingwa msimu ujao. Vilabu vingine kama Tottenham Hotspur na Inter Milan pia vinatajwa kufuatilia kwa karibu hali yake.

Licha ya ofa hizi zote, Goretzka bado ameweka kipaumbele chake kwa sasa kumalizia msimu na Bayern na kushiriki Kombe la Dunia lijalo. Baada ya hapo, ataamua hatma yake na bila shaka, uamuzi huo unaweza kuwa moja ya sajili kubwa zaidi ya majira ya joto.

