Guardiola: Cancelo alihitaji Muda Zaidi wa Kucheza

Kocha wa klabu ya Manchester City Pep Guardiola amesema sababu ya kuondoka kwa bei wa klabu hiyo raia wa kimataifa wa Ureno ni kutokana kwa mchezaji huyu kuhitaji nafasi ya kucheza zaidi.

Guardiola amesisitiza kua mchezaji huyo ameamua kuondoka klabuni hapo na kuelekea klabu ya Fc Bayern ili kupata nafasi ya kucheza zaidi, Kwani mchezaji huyo anahitaji kucheza kila mchezo kitu ambacho amekua hakipati ndani ya klabu ya Manchester City.GuardiolaMchezaji Joao Cancelo ameondoka ndani ya klabu ya Manchester City na kuelekea klabu ya Bayerrn Munich ya nchini Ujerumani kwa mkopo wa nusu msimu, Mchezaji huyo atakua akiitumikia klabu ya Bayern Munich kwa mkopo mpaka mwishoni mwa msimu huu huku kukiwa na kipengele cha kununuliwa na klabu ya Bayern Munich kwa mkataba wa kudumu.

Pep Guardiola amesema kua hajui nini kitaendelea msimu ujao baina ya klabu hiyo na mchezaji Joao Cancelo, Kauli hii ya kocha huyo inatoa picha ya tofauti baina ya klabu hiyo na mchezaji wake kwani inawezekana mchezaji huyo akajiunga na klabu ya Bayern Munich kwa uhamisho wa kudumu.GuardiolaKocha Guardiola amesema hawezi kuangea neno baya kwa mchezaji huyo kwani amekua na uwezo mkubwa, nidhamu ya kazi, kujitoa kwa hali ya juu. Ni wazi Cancelo ni mchezaji ambae kocha huyo bado anahitaji kua nae kwenye kikosi chake lakini baada ya maneno ya kocha huyo inaonesha kua kocha huyo hana tataizo na mchezaji huyo kama ambavyo ilikua inaelezwa mwanzo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.