Meneja wa Manchester City, Pep Guardiola ameeleza umuhimu wa ushindi wa 1-0 dhidi ya Chelsea uwanjani Etihad lakini akasisitiza kuwa taji la Ligi Kuu ya Uingereza huwezi kushinda mwezi Januari.

 

guardiola, Guardiola : Hakuna Ubingwa wa January., Meridianbet

Kevin De Bruyne alifunga bao lake la tano dhidi ya klabu yake ya zamani, Chelsea zikiwa zimesalia dakika 20 uwanjani Etihad kupata ushindi dhidi ya mabingwa hao wa Ulaya.

“Ushindi muhimu kwa sababu tunacheza dhidi ya mshindani mkubwa,” Pep Guardiola alisema. “Unapopata pointi tatu, hawawezi kupata pointi tatu na ni wiki moja pungufu.

“Lakini Januari hakuna bingwa. Tunaweza kufikiria kuhusu Chelsea, na Liverpool wana mechi mkononi. Wakishinda itakuwa na pointi nane na pointi nane Januari si kitu.

“Nataka kushinda endapo tunastahili, na tulistahili. Ninapenda soka kuwa la haki kwahiyo, wakati nilikuwa na furaha kushinda dhidi ya Arsenal, hatukustahili. Kushinda wakati wa unastahili hujisikia vizuri.” aliongeza Guardiola.


JIACHIE NA ALMIGHTY AZTEC

Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa