Guimaraes Hana Mpango wa Kuondoka Newcastle

Kiungo wa kimataifa wa Brazil anayekipiga ndani ya klabu ya Newcastle United Bruno Guimaraes amesema hana mpango wa kuhama ndani ya klabu hiyo kwakua anataka kutengeneza historia klabuni hapo.

Bruno Guimaraes ambaye alikuja ndani ya klabu ya Newcastle United tangu msimu uliomalizika akitokea klabu ya Olympique Lyon, Ameahidi kuhitaji kusalia ndani ya klabu ya Newcastle licha ya klabu hiyo kutoshiriki ligi ya mabingwa ulaya lakini mchezaji huyo anaamini klabu hiyo itashiriki michuano hiyo sana siku za mbele.GuimaraesKiungo huyo anaiona klabu ya Newcastle ikicheza michuano ya ulaya mara kwa mara kwani klabu hiyo imekua kwenye mradi mzuri wa kuitengeneza klabu hiyo ili ije kufanya vizuri siku za mbeleni, Kiungo huyo amekua kwenye kiwango bora sana ndani ya klabu hiyo na anaaamini timu hiyo itafanya vizuri siku za usoni.

Kiungo Bruno Guimaraes pia amemzungumzia kocha Pep Guardiola na baada ya kocha huyo kumwambia yeye ni mchezaji mzuri, Huku yeye akilichukulia jambo hilo chanya sana na kumfanya kua na furaha kwasababu kocha huyo ni kocha bora kwake ambaye amewahi kumtazama.GuimaraesKiungo Bruno Guimaraes pia amemzungumzia kocha wa klabu yake kwasasa Eddie Howe na kuamini kocha huyo atakua kocha wa timu ya taifa ya Uingereza, Kwani kocha huyo amekua moja ya makocha bora sana wakiingereza wanaofanya vizuri na hilo ni jambo ambalo limemfanya kiungo huyo kuamini kua kocha huyo anaweza kuifundisha timu ya taifa ya Uingereza.

 

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.