Wachezaji IIkay Gundogan na Phil Foden walikuwa wachezaji waliozamisha jahazi la Liverpool uwanjani Anfield baada ya kukubali kipigo cha 4-1 kutoka kwa Manchester City.
Ukiachana na kile mashabiki wa Liverpool wanachokiita Laana ya City kushindwa kushinda katika dimba la Anfield lakini hali ilikuwa tofauti katika mchezo wao wa jana.
Gundogan alikosa penati katika kipindi cha kwanza kabla ya kufunga dakika ya 49′ na 73′ ya mchezo wakati Sterling na Foden wakizamisha chombo dakika ya 76′ na 83′ mtawalia.

City wanaongoza jedwali la Epl wana alama 50 mbele ya Liverpool waliokatika nafasi ya 4 wakiwa na alama 40. Timu hizo zimekuwa timu bora katika misimu minne iliyopita na kuwa na upinzani mkubwa.
Citizen walikuwa bila ya wachezaji wao Kelvin de Bruyne na Sergio Aguero huku wakianza mchezo wa jana bila ya mshambuliaji yeyote na kufanikiwa kupata magoli manne.
IIkay Gundogan amekuwa na fomu nzuri katika mechi 12 zilizopita akifanikiwa kufunga magoli 12, wakati City wakiwa hawajapoteza katika michezo 13 iliyopita.
Unaweza kuvuna mkwanja mrefu kadiri uwezavyo kupitia mchezo wa Gold n Rocks kwenye kasino ya mtandaoni ya Meridianbet. Ni rahisi! Vigezo na masharti, kuzingatiwa.



warda
Jamani Man U nao wapate nafasi
Ernest Kimeru
Vijana wa Pep wanatumia chance ya kujihakikishia wanakuwa mabingwa msimu huu japokuwa ushindano mkunwa lakini City wanaonekana kuwa na kikosi kipana sana na kuwapa advantage ya kuwa mabingwa msimu huu
Magdalena
Wamejua kuwachakaza Liverpool ilikuwa balaa
Khadija
Asante kwa taarifa
Venerose
Goods news
Rahma
Habari njema
Dorophina
Liverpool wameanza kuzama taratibu
Hopemwaikuka
Kaz ipo
Angelina
Wanakibarua kizito
Mwanahamisi
Kazi ipo
Sania
Hiki ni kipindi kigumu kwa Liverpool
lombo
asante meridianbet kwa habar moto moto
Sarah
Mh hatari
Lydia Emmanuel Magoti
Habari nzuri