Gyökeres Aibeba Sweden Kwa Kufunga Hat-trick Muhimu

Mshambuliaji Viktor Gyökeres alikuwa shujaa wa Sweden usiku wa Alhamisi baada ya kufunga hat-trick iliyowapa ushindi wa 3-1 dhidi ya Ukraine. Matokeo hayo yanaweka hai ndoto za Sweden kufuzu Kombe la Dunia 2026, huku sasa wakijiandaa kwa mechi ya mtoano dhidi ya Poland itakayotoa mshindi wa mwisho.

Gyökeres Aibeba Sweden Kwa Kufunga Hat-trick Muhimu

Katika mchezo mkali uliopigwa Valencia, Gyökeres alionyesha ubora wake mapema kabisa, akifunga bao la kwanza dakika ya 6 kwa shuti la karibu. Bao hilo lilituliza presha kwa Sweden na kuweka msingi wa kiwango bora alichoonyesha mshambuliaji huyo katika mchezo mzima.

Hakusimama hapo, kwani mwanzoni mwa kipindi cha pili aliongeza bao la pili kwa umakini mkubwa, akionesha utulivu na uwezo wa hali ya juu. Baadaye alijipatia penalti na kuifunga mwenyewe dakika ya 73, akitimiza hat-trick yake. Bao la Matvii Ponomarenko kwa Ukraine lilikuwa la kufutia machozi tu.

Gyökeres Aibeba Sweden Kwa Kufunga Hat-trick Muhimu

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Ushindi huu ni hatua muhimu kwa Sweden baada ya kuanza vibaya kampeni ya kufuzu. Kocha Graham Potter ameonekana kupata mfumo sahihi, akimtumia Gyökeres kama mhimili wa ushambuliaji, jambo lililoifanya timu ionekane imara zaidi kuliko awali.

Gyökeres Aibeba Sweden Kwa Kufunga Hat-trick Muhimu

Sasa macho yote yanaelekezwa kwenye pambano la mwisho dhidi ya Poland jijini Stockholm. Poland walifuzu hatua hiyo baada ya kuifunga Albania 2-1. Mshindi wa mechi hiyo atapata tiketi ya kushiriki Kombe la Dunia 2026 litakalofanyika Marekani, Mexico na Canada.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.