Mshambuliaji wa klabu ya Manchester City Earling Haaland amefanikiwa kufunga mabao matano katika mchezo wa ligi ya Mabingwa ulaya usiku wa jana dhidi ya Rb Leipzig na kufanikiwa kufikia rekodi ya Lionel Messi.
Earling Haaland alikua na usiku wa aina yake katika ushindi wa mabao 7-0 walioupata klabu ya Manchester City dhidi ya klabu ya Rb Leipzig, Huku mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Norway akifanikiwa kuweka rekodi tofauti tofauti katika mchezo wa jana.
Klabu ya Manchester City ilifanikiwa kuingia hatua ya robo fainali kwa staili ya aina yake baada ya kuiangamiza klabu ya Rb Leipzig kwa kichapo kizito cha mabao 7-0, Huku mshambuliaji wao matata akiweka rekodi baada ya kufunga mabao matano peke yake katika mchezo huo.
Earling Haaland jana alifanikiwa kufunga mabao matano katika hatua ya mtoano ya ligi ya mabingwa ulaya akiwa mchezaji wa pili baada ya Lionel Messi kufanya hivo mwaka 2012 dhidi ya klabu ya Bayern Leverkusen kutoka nchini Ujerumani, Hii inamfanya mshambuliaji huyo kuingia kwenye vitabu vya historia.
Mshambuliaji Earling Haaland amefanikiwa kuvunja rekodi nyingine siku ya jana baada ya kua mchezaji wa kwanza kufunga mabao 30 katika michezo michache zaidi ya ligi ya mabingwa ulaya, Mshambuliaji huyo jana alifanikiwa kufikisha mabao 30 katika michezo michache zaidi akiwa amecheza michezo 25 tu akivunja rekodi ya Ruud Van Nistelrooy aliefikisha mabao 30 kwa michezo 34.

