Liverpool Kurudia ya Barcelona kwa Madrid Leo?

Klabu ya Liverpool itashuka dimbani leo kumenyana na klabu ya Real Madrid katika mchezo wa ligi ya mabingwa barani ulaya hatua ya 16 bora ili kuhakikisha wanaweza kupindua matokeo baada ya kufungwa mabao 5-2 nyumbani.

Klabu ya Liverpool inasubirirwa kufanya miujiza kama ambavyo wamekua wakifanya mara kadhaa katika michezo yake, Klabu hiyo iliwahi kupoteza kwa mabao matatu kwa bila dhidi ya klabu ya Barcelona, Lakini iliweza kupindua matokeo katika dimba la Anfield na kushinda kwa mabao manne kwa bila na kufanikiwa kutinga hatua ya fainali.LiverpoolReal Madrid wanafaida kubwa kwani tayari wamefanikiwa kushinda kwa mabao matano kwa bila katika dimba la Anfield wiki mbili zilizopita kwa mabao matano kwa mawili, Lakini tofauti hiyo ya mabao ndio ilikua dhidi ya Barcelona mwaka 2019 lakini vijogoo wa Anfield walifanikiwa kupindua matokeo.

Klabu ya Liverpool imekua na kawaida ya kupindua matokeo ambayo wanakua wametanguliwa katika michezo yake wakifanikiwa kufanya hivo mbele ya Barcelona mwaka 2019, Lakini mwaka 2005 wakifanya hivo mbele ya wababe wa Italia klabu ya Ac Milan baada ya kutanguliwa kwa mabao matatu kwa bila kipindi cha kwanza na kufanikiwa kuchomoa yote kipindi cha pili na kushinda kwa mikwaju ya penati.LiverpoolKlabu ya Real Madrid wao wameeleza kua wanatambua mchezo dhidi yao na Liverpool haujamalizika na wanakwenda kwenye mchezo huo wakiwa na akili ya kutambua mchezo huo unaanza upya kwa maana ya 0-0, Kwani wanajua ubora wa miamba hiyo ya Anfield katika kupindua matokeo wakifanya hivo katika michezo tofauti tofauti.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.