Guardiola Aivulia Kofia Napoli

Kocha wa klabu ya Manchester City Pep Guardiola ameonekana kuikubali klabu ya Napoli na kusema ni klabu bora kwasasa barani ulaya kutokana na aina yao ya uchezaji, Ikiwa inakaribiana na klabu ya Arsenal.

Kocha Guardiola amezungumza hayo baada ya mchezo wa jana dhidi ya klabu ya Leipzig ambapo walishinda kwa mabao 7-0 na kufanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa ulaya baada ya kutoa kipigo hicho kizito kwa klabu ya Rb Leipzig.guardiolaKlabu ya Napoli imekua na msimu bora ikiwa imefanikiwa kutengeneza pengo kubwa la alama baina yake na vilabu vingine katika ligi kuu ya Italia ikiwa kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo, Huku pia ikiwa kwenye michuano ya ligi ya mabingwa ulaya hatua ya 16 bora tayari wakiwa na faida ya mabao mawili ya ugenini dhidi ya Frankfurt.

Kocha Guardiola anaamini Napoli ni moja ya klabu bora sana kwasasa barani ulaya ikiwa na inashahabiana na klabu ya Arsenal ambayo pia ni vinara wa ligi kuu ya Uingereza wakifanikiwa kuonesha kiwango bora sana, Hivo kocha huyo anaviona vilabu hivo kama vilabu bora kwasasa kwenye bara la ulaya.guardiolaKlabu ya Napoli na Arsenal wpte wanaongoza ligi zao za nyumbani wakifanikiwa kuwashangaza watu wengi kwani sio timu ambazo zilipewa nafasi kufanya vizuri, Lakini mpaka sasa ni vilabu ambayo vimeonesha ubora mkubwa na kufanikiwa kuongoza ligi zao kutokana na uwezo wanaouonesha.

Acha ujumbe