Haaland: Nilitaka Kufunga Zaidi

Mshambuliaji wa klabu ya Manchester City Earling Haaland amesema alitaka kufunga mabao zaidi ya matano katika mchezo wa jana dhidi ya klabu ya Rb Leipzig lakini hakua na namna zaidi baada ya kufanyiwa mabadiliko.

Haaland anasema alimuambia kocha Pep Guardiola wakati anamfanyia mabadiliko kua alihitaji kufunga Hattrick mbili katika mchezo wa jana, Mchezaji huyo hadi anatoka dakika ya 63 alikua tayari ameshafunga mabao matano hivo alihitaji bao moja kufikisha Hattrick mbili.HaalandMshambuliaji huyo alifanikiwa kuweka rekodi tamu katika mchezo wa jana kwani alifanikiwa kua mchezaji wa kwanza kufunga mabao 30 katika michezo michache zaidi, Kwani mshambuliaji huyo amefanikiwa kufunga mabao 30 ndani ya michezo 25 tu akivunja rekodi ya Ruud Van Nistelrooy aliefikisha ndani ya michezo 34.

Mshambualiaji Haaland amefurahishwa na kufunga mabao matano ndani ya mchezo mmoja kwenye hatua ya mtoano ya ligi ya mabingwa ulaya, Lakini bado alionesha kusikitishwa kutokana na nafasi mbili alizozikosa katika mchezo huo katika kipindi cha kwanza.HaalandHaaland ameonesha ni mchezaji mwenye njaa ya kufunga mabao kwani licha ya kufunga mabao matano katika mchezo huo ila alihitaji kufunga zaidi, Hii imemfanya kocha wake Pep Guardiola kuamini kua mchezaji huyo atakuja kufanya mambo makubwa siku za usoni akiendeleza anachofanya.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.