Haaland: Kila Kinachofanywa sasa Pele Alishakifanya

Mshambuliaji wa klabu ya Manchester City Earling Braundt Haaland amesema kua kila kinachofanywa na mchezaji yeyote wa sasa kimeshafanywa na gwiji Pele.

Baada ya kifo cha gwiji wa soka duniani Edison Arantes Do Nascimento ndipo mchezaji wa klabu ya Manchester City Haaland kuandika kwenye kurasa zake za kijamii kua kila kinachofanywa na mchezaji yeyote basi gwiji Pele alikifanya wakwanza.haalandKufuatia kauli hiyo ya mshabuliaji huyo inaonesha namna gani ana heshima juu ya gwiji huyo wa soka duniani ambaye amefariki jana akiwa na umri wa miaka 82, Pele anatajwa kama mchezaji bora wa muda wote duniani kuwahi kutokea kutokana na mambo ambayo amefanikiwa kufanya katika mpra wa miguu.

Gwiji Pele ambaye alikua anasumbuliwa na saratani kwa muda mrefu amefariki dunia usiku wa jana na kusababisha simanzi duniani kote kutokana na makubwa aliyoyafanya kwenye mpira wa miguu, Pia gwiji huyo atakumbukwa kama mchezaji pekee kushinda mataji matatu ya kombe la dunia.haalandPele amefanya mengi kwenye ulimwengu wa mpira wa miguu na kumfanya Haaland kukiri kua wanayoyafanya kwasasa wao ni marudio tu, Mshambuliaji huyo alimalizia kwa kusema Pele ni mfalme wa mpira wa miguu na hii ilithibitika kwani mchezaji huyo anashikilia tuzo ya mchezaji bora wa karne iliyotolewa na Fifa.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.