Hawa Hapa Waliofuzu EURO 2024 Huko Ujerumani

Tayari kuna timu 17 zilizohakikishiwa kufuzu EURO 2024, ikiwa ni pamoja na wenyeji Ujerumani, lakini droo ya Desemba 2 inategemea matokeo ya kufuzu na sio kuorodheshwa.

 

Hawa Hapa Waliofuzu EURO 2024 Huko Ujerumani

Italia itaungana na timu hizo katika kutafuta kufuzu ikiwa watafanikiwa kuepuka kushindwa dhidi ya Ukraine leo hii huko Leverkusen.

Wenyeji Ujerumani na timu mbili za juu kutoka kwa kila kundi wana uhakika wa kupata ufikiaji, pamoja na timu nyingine tatu ambazo zitafuzu EURO kupitia mchujo.

Kwa kuwa mechi hizo za mchujo hazitachezwa hadi Machi 2023, ina maana kwamba droo ya michuano hiyo Desemba 2 itakuwa na nafasi tatu kwa timu zitakazopitia njia hiyo.

Hawa Hapa Waliofuzu EURO 2024 Huko Ujerumani

Badala ya kutumia mfumo wa viwango vya FIFA au UEFA, droo inatokana na matokeo ya kufuzu, kwa hivyo wale wote wanaoingia kwenye mchujo wako kwenye Chungu cha 4

Kuna timu 12 zinazoingia kwenye hatua ya mtoano, lakini ni timu tatu pekee ndizo zitafuzu dimba hilo baada ya mikwaruzano ya nusu fainali na fainali.

Droo ya mechi za mchujo itafanywa mjini Nyon mnamo Novemba 23.

Waliofuzu tayari EURO 2024 ni pamoja na;

Hawa Hapa Waliofuzu EURO 2024 Huko Ujerumani

Ujerumani (wenyeji), Albania, Austria, Ubelgiji, Denmark, Uingereza, Ufaransa, Hungaria, Uholanzi, Ureno, Romania, Scotland, Serbia, Slovakia, Hispania, Uswizi, Uturuki

Wanaoelekea kwenye Mechi za Mchujo ni pamoja na; Georgia, Ugiriki, Kazakhstan Luxemburg, Israel, Bosnia na Herzegovina, Poland, Wales, Estonia

Acha ujumbe