Aston Villa tayari wamemkaribisha Jack Grealish mazoezini wakati staa huyu akihusishwa zaidi na uhamisho wa kwenda Manchester City.
Nyota huyu amefurahia likizo ndefu baada ya kukamilisha kibarua chake kwenye Euro 2020, huku chini ya kapeti kukiwa na habari za nia za timu za EPL kuiwinda saini yake.
Villa wanatajwa kuwa tayari kupokea ofa ya £100m, kwa ajili ya uhamisho wa staa huyu.
Kupitia ukurasa wa Twitter wa Aston Villa wameonesha Grealish akiungana na kikosi cha kwanza kwenye mazoezi ya Pre-season.

Taarifa zinasema kuwa mamlaka za klabu zinaendelea kuangalia namna ya kushughulikia suala la mchezaji huyo wakiamini wanaweza kumshawishi asalie kwa mshahara wa £200,000 kwa wiki.
Wakati huo Manchester City wanatarajia Jack Grealish awasilishe ombi la uhamisho klabuni hapo. City pia wanahusishwa na Harry Kane wa Tottenham, ambaye anaripotiwa kuwa hajawasili mazoezini licha ya kutakiwa kuwasili leo kwa ajili ya mazoezi ya Pre-season.
Unakila sababu ya kuwa moja ya mamilionea katika kasino za mtandaoni za meridianbettz, Mchezo wa Ruby Casino Queen unaweza kukufanya ujishindie mkwanja mrefu. Furahia ubora wa kasino zetu na njia kibao za kuwa mshindi leo hii ukiwa na mrembo Ruby.!


