James Maddison Nje Mwezi Mmoja Mpaka Mitatu

Kiungo wa klabu ya Tottenham na timu ya taifa ya Uingereza James Maddison anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa muda unaokadiriwa mwezi mmoja mpaka mitatu.

James Maddison alipata majeraha katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza uliopigwa Jumatatu dhidi ya klabu ya Chelsea na kumfanya kushindwa kumaliza mchezo huo.james maddisonKiungo huyo inaelezwa majeraha ya enka ndio yatamfanya mchezaji huyo kukaa nje ya uwanja kwa muda wa mwezi mmoja mpaka miezi mitatu, Huku klabu ya ikionekana kupitia kipindi kigumu kwasasa kutokana na majeraha.

 

Klabu ya Totenham mbali na kiungo huyo wa kimataifa wa Uingereza lakini klabu hiyo imekua ikiandamwa na majeraha, Kwani wachezaji kama Richarlison, matty Van de Vien, Ivan Perisic na Pedro Porro nao wanaelezwa kupata majeraha.james maddisonKiungo James Maddison amekua na mchango mkubwa tangu ajiunga na klabu ya Tottenham akitokea Leicester City, Kwani mpaka sasa amekua moja ya wachezaji waliohusika na mabao mengi ndani ya klabu hiyo.

Acha ujumbe