Januari Imeisha Kibabe Sokoni.

Mchongo wa usajili wa dirisha dogo mwezi Januari umetamatika usiku wa kuamkia leo. Wapo waliolamba dume na wapo waliotoka patupu.

Sakata la wiki 7 za sintofahamu ndani ya Arsenal, zimetamatika. Pierre-Emerick Aubameyang ameondoka Emirates na kujiunga Barcelona. Huu ni usajili ambao, Aubameyang amevunja mkataba wake wa miezi 18 iliyosalia na Arsenal ili ajiunge na Barca. Wakati huohuo, Arsenal hawajasajili mchezaji yeyote Januari hii.

Man United imefungua milango kwa wachezaji watatu wa kikosi cha kwanza. Martial, Van De Beek na Amad wametolewa kwa mikataba ya mkopo. Jones aligoma kwenda Boudeux licha ya United kukubaliana na biashara hiyo. Jesse Lingard pia amejikuta akibaniwa kuondoka United licha ya West Ham na Newcastle kuweka ofa mezani.

Chelsea hawajauza wala kununua kwenye dirisha hili. Wachezaji wa kikosi cha kwanza wapo vilevile. Man City imemvuta Julian Alvarez kutokea River Plate lakini, mchezaji huyo atabaki Plate mpaka mwezi Julai mwaka huu.

Liverpool wamemvuta Luis Diaz kutokea FC Porto na kuongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji. Dakika za mwisho, wameshuhudia usajili wa Fabio Carvalho ukikwama kukamilka ndani ya muda kutokea Fulham.

Spurs wameshusha wawili, Rodrigo Bentacur na Dejan Kulusevski kutokea Juventus. Wakati huo huo, Tanguy Ndombele, Delle Alli, Bryan Gil na Giovani Lo Celso wakiondoka klabuni hapo.

Newcastle imesajili jumla ya wachezaji watano, Everton imempa Frank Lampard nafasi ya kuiongoza timu hiyo, Christian Eriksen amerejea kwenye EPL akiwa ni mchezaji halali wa Brentford. Phillippe Coutinho ametua Villa Park akifanya kazi na Steven Gerrard kama kocha na mchezaji. Hakika, Januari imeisha kibabe sokoni.


VUNA MKWANJA NA KENO

Dakika tano pekee zinakutosha kuwa mmoja wa washindi wa mkwanja mrefu ndani ya kasino pendwa ya meridianbettz katika sloti maridhawa ya KENO, moja ya michezo inayoipa thamani dau lako.

tetesi, Tetesi za Soka barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe