Sakata la Mason Greenwood: United Waondoa Bidhaa Zake Sokoni

‘Mwanakulisaka, Mwanakulipata’ inafaa kumwambia Mason Greenwood ikiwa atapatikana na madai yanayotajwa juu yake.

Klabu ya Manchester United imeondoa bidhaa zote za Mason Greenwood kwenye soko la mtandaoni la klabu hiyo kutokana na madai yanayomlenga fowadi huyo.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 20 amekamatwa kwa tuhuma za ubakaji na unyanyasaji kufuatia madai yaliyotolewa na mpenzi wake katika mitandao ya kijamii ikiwa ni pamoja na picha na sauti.

Man United imemsimamisha mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza, ambaye hataruhusiwa kufanya mazoezi na timu au kushiriki katika mechi hadi hapo itakapotangazwa vinginevyo.

Polisi wa Manchester walithibitisha kuwa wamemkamata siku ya Jumapili, huku staa huyo aliye na umri wa miaka 20 akiwekwa kizuizini, ambapo alikaa usiku kucha kwa mahojiano.

The Red Devils sasa wamehakikisha bidhaa za Greenwood zisipatikane kwenye manunuzi kwenye duka lao la mtandaoni.

Man United itarejea uwanjani kumenyana na Middlesbrough katika mchezo wa raundi ya nne ya Kombe la FA Ijumaa jioni, lakini Greenwood hatashiriki katika kikosi cha Ralf Rangnick.


 

VUNA MKWANJA NA KENO

Dakika tano pekee zinakutosha kuwa mmoja wa washindi wa mkwanja mrefu ndani ya kasino pendwa ya meridianbettz katika sloti maridhawa ya KENO, moja ya michezo inayoipa thamani dau lako.

tetesi, Tetesi za Soka barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe